LIGI KUU ENGLAND STAMFORD BRIDGE: MAN UNITED YAPIGWA 3-1, UBINGWA….BAI BAI??

Sunday, 19 January 2014 20:59 E-mail Print PDF >>WADAU WADAI KILICHOBAKI SASA NI KUPIGANIA 4 BORA TU! >>HETITRIKI YA GWIJI WA CAMEROUN, ETO’O, YAIUA UNITED! MATOKEO Jumapili Januari 19 Swansea 1 Tottenham 3 Chelsea 3 Man United 1 ++++++++++++++++++++++ ETOO_IN_CHELSEA2MABINGWA Manchester United walitawala Kipindi cha Kwanza na kujikuta wako nyuma kwa Bao 2-0 dhidi ya Chelsea, Bao zote zikifungwa na Gwiji wa Cameroun Samuel Eto’o, kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Stamford Bridge waliyomaliza kwa kipigo cha Bao 3-1 ambacho kwa Wadau wao huenda kimehakikisha kwamba hawawezi tena kutetea Taji lao kwani sasa wako Pointi 14 nyuma ya Vinara Arsenal huku zimebaki Mechi 16. Pengine kilichobaki kwao sasa ni kuwania kumaliza ndani ya 4 bora ili wafuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao kwani wapo Pointi 6 tu nyuma ya Nafasi hiyo ya 4. Chelsea walipata Bao lao la kwanza katika Dakika ya 17, bila kutegemewa kwani Man United ndio waliokuwa juu kimchezo, baada ya uzembe wa kutomkaba Samuel Eto'o ambae alipokea Mpira wa kurushwa na kumhadaa kirahisi Phil Jones kisha kupiga Shuti la Mita 20 na kumbabatiza Mchael Carrick na kumpoteza Kipa De Gea. Bao la Pili lilifungwa kwenye Dakika ya 45 na Eto’o kufuatia ulinzi duni baada Kona kupigwa na kuokolewa na Mpira kumkuta Ramires aliempasia Cahill aliemsogezea Eto’o na kupachika kilaini. Bao la 3 lilipigwa tena na Eto’o, ni Hetitriki kwake, kufuatia Kona ya Dakika ya 49 iliyounganishwa na Cahill na kuokolewa na De Gea na kutua miguuni mwa Eto’o ambae alimalizia kilaini kwa mara nyingine. Javier Hernandez ‘Chicharito’ aliifungia Bao lao pekee Man United katika Dakika ya 78 kufuatia kazi njema ya Danny Welbeck kumfikia Phil Jones ambae shuti lake lilionekana kutokuwa na madhara hadi alipochomoza Chicharito. Man United walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada Nahodha wao Nemanja Vidic kupewa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya kwa Eden Hazard.
VIKOSI: CHELSEA: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Luiz, Willian, Oscar, Hazard, Eto'o Akiba: Cole, Lampard, Torres, Mata, Mikel, Matic, Schwarzer.
MAN UNITED: De Gea, Rafael Da Silva, Evans, Vidic, Evra, Jones, Carrick, Valencia, Januzaj, Young, Welbeck Akiba: Giggs, Smalling, Lindegaard, Hernandez, Cleverley, Fletcher, Kagawa.

0 comments:

Post a Comment

Top 10 Articles

Gallery

PGA Head Teaching Professional

Portfolio